Skip to main content
News and Events

Waziri Mahiga ampokea Waziri wa Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akimpokea rasmi Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Jean-Marc Ayrault (kushoto) alipotembelea Wizarani katika ziara yake ya kikazi nchini. Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa ili kuchangia  maendeleo ya nchi hizi mbili. Pia Waziri Mahiga alitumia fursa  hiyo kumpa salamu za pole kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyotokea nchini Ufaransa hivi karibuni. Mazungumzo hayo yalifanyika  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2016.