Skip to main content
News and Events

Waziri Mahiga Akutana na Waziri wa Korea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augistine Mahiga (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Mipango na Uratibu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea, Mhe. Balozi Paik Ji-ah. Mazungumzo yao yalijikita katika kukuza mahusiano baina ya Tanzania na Korea Kusini katika nyanja za   miundombinu, biashara na afya. Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi Paik kwa ushirikiano wanaouendeleza katika kuisaidia Tanzania ikiwemo mchango wao kwenye ujenzi wa Daraja la Malagarasi huko Kigoma na miradi mingine ya barabara.Mhe. Balozi Ji-ah yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.