WAZIRI KABUDI AMUAGA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akimkabidhi zawadi Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam. Waziri Kabudi katika hotuba yake amempongeza Bwana Rodriguez kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chote akiwa nchini. Aidha, amemshukuru kwa kushirikiana na Serikali na kujitoa kwa dhati katika kuchangia juhudi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali nchini. Bwana Rodriguez amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini Tanzania ambapo amefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano.

WAZIRI KABUDI AMUAGA  MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

  • Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, anayemaliza muda wake wa kuhudumu nchi wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga
  • Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wa kuhudumu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi kutoka wizarani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa