Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 20, 2019
Bw. Zuberi Kachingwe Afisa Usafirisahaji, IKULU,(katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua magari yatakayotumiwa na viongozi na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujiridhisha juu ya matayarisho ya mapokezi kwa ajili ya mkutano huo utakaofanyika Dar es Salaam,Tanzania. Kulia ni Afisa Usafirishaji Msaidizi Bw. Athumani Natepe. August 8, 2019.
Mazungumzo yakiendelea