WAZIRI KABUDI AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI

Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Waziri Kabudi katika Mkutano wake na wanahabari amewashukuru nakuwapongeza waandishi wa habari na vyombo vya habari, kwa ushirikiano mkubwa na uzalendo waliouonyesha katika kuutangaza Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Waziri Kabudi alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kuendelea kufuatilia na kuuhabarisha umma masuala mbalimbali yanayojiri kweny ya Jumuiya SADC. Tanzania itaendelea kuwa mwenyeji wa Mikutano mbalimbali ya kisekta ya SADC katika kipindi cha hiki cha mwaka mmoja cha Uenyekiti wake.

WAZIRI KABUDI AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI