Skip to main content
News and Events

Waziri apokea Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na kufanya mazungumzo naye.

  • Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 16 Septemba, 2016.