Skip to main content
News and Events

UJUMBE WA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA SGR

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo unaotekelezwa hapa nchi. Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote ulianza safari ya kutembelea mradi huo kuanzi Makutopola hadi Dar es Salaam. Ujumbe ulipate fursa ya kujionea hatau ya maendeleo iliyofikiwa sambamba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na katika utelezaji wa mradi, ikiwemo viwanda vya kuzalishia baadhi vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa mradi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Eng. Mlote amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kutekeleza mradi huo ambao unamanufaa makubwa kwa Taifa na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. “tuemona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteleza mradi huu mkubwa, tunampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kubuni mradi huu.” Eng.Mlote. Aidha, aliongezea kusema amefurahishwa na ushiriki wa idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania katika sekta mbalimbali za ujenzi wa mradi huo ulioajiri takribani watu 13,796. Amewasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujunzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza mradi huo hata baada ya wataalmu kutoka kampuni inayohusika na ujenzi kuondoka nchi. 

Kwa upande mwingine Eng. Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la mrafi, wikuanza kujiandaa kikamilifu katika kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi wa reli ya kisasa kwa kuanza kuongeza uzalisha wa mazao shambani na bidhaa za viwandani kwa kuwa mradi huo utarahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kwenda nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nchi za Afrika ya Kati. 

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pia unatarajia kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, lililopo Wilayani Rufiji kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi.

  • Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu alipotembelea moja ya handaki (tunnel) ya kupita treni ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi.Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu alipotembelea moja ya handaki (tunnel) ya kupita treni ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi.
  • Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi. Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi.