Ubalozi wa Pakistan nchini Waadhimisha Miaka 76 ya Uhuru
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akitoa hotuba kama mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 76 ya Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan. Katika hotuba yake Balozi Mwinyi alielezea historia ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo ulioanza tangu mwaka 1967 chini ya usimamizi wa Waasisi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.