Rais Paul Kagame wa Rwanda awasili Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mhe. Paul Kagame yupo nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo, ambapo anatarajiwa kufungua Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam