Prof. Kabudi aviomba vyombo ya habari kuelimisha umma kuhusu SADC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere leo. Prof. Kabudi aliwaeleza Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini mwezi Agosti 2019. Prof. Kabudi aliwasihi Wakuu hao kushirikiana na Serikali hususan katika kueleimisha umma kuhusu SADC pamoja na kutoa elimu kwa wafanaybiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu fursa za mkutano huo za zile zinazopatikana katika nchi wanachama wa SADC.
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akitoa neno katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Prof. Kabudi azungumze na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Dkt. Abbas al
Baadhi ya Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini walioshiriki katika kikao cha Waziri. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Dkt. Ayoub Rioba.
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini.