Mkutano wa 9 wa Tume ya Pamoja kati ya Tanzania na India Uliofanyika New Delhi ,India
Mkutano wa 9 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India Ngazi ya Mawaziri Uliofanyika mjini New Delhi, katika Mkutano huo uliotanguliwa na Mkutano wa Ngazi ya wataalamu wakiongozwa na Makatibu Wakuu Tarehe 15 na Tarehe 16 Octoba Ngazi ya Mawaziri.
Pia katika Mkutano huo Serikali ya Tanzania na India ziliwekeana saini kwenye mikataba miwili, ukiwepo Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na India kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi na Mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya India (NRDC).
Aidha, Ujumbe wa Tanzania Uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Justa Nyange, na viongozi kutoka kwenye Taasisi.