Skip to main content
News and Events

Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wafikia tamati

Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ulikuwa na ujumbe na uwakilishi kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. .

Rais Mhe. Dkt. Magufuli akizungumza katika Mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya.

Aidha mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mhe. Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kunakila sababu ya kulinda na kudumisha Mtangamano kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama.

Pia Mkutano huu wa 18 wa Wakuu wa nchi umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Eng. Steven Mrote kutoka Tanzania.


Katika Kutano huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi rasmi uwenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini moja ya nyaraka ya makabidhiano ya uwenyekiti wakati wa Mkutano wa 18 wa Kaiwa wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki
  • Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)
  • Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Aziz P. Mlima (kulia) akifuatilia Mkutano
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), naye akisalimiana na Waziri Nak-Yon mara baada ya kupokelewa na Mhe. Majaliwa, wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwele naye akisubiria kusalimiana na Waziri Mkuu wa Korea.
  • Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samuel Shelukindo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
  • Waziri Mhe. Mahiga akifuatilia Mkutano
  • Picha ya pamoja