MABALOZI WA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Jengo la Makumbusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea jengo hilo Agosti 19, 2019.

MABALOZI WA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

  • Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (katikati; ambaye pia aliongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara) akitoa maelezo kwa Mabalozi waliopotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Jumla ya mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani wapo nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Wakiwa Zanzibar Mambalozi wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall), uwanja mpya wa ndege (terminal 3), ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Fumba, ujenzi wa mradi wa barabara ya kilomita 31 (Kitope hadi Mkokotoni) na ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo eneo la Mnangapwani. Mabalozi wamendelea kuridhishwa na kufahishwa na namna Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) zilivyo jidhatiti kutekeleza miradi mikubwa ambayo itachagiza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
  • Ujenzi wa daraja ukiendelea katika barabara ya Kitope-Mkokotoni
  • Mabalozi wakisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Zanzibar (Tereminal 3), kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo Bw. Yasiri Costa.
  • Mabalozi wakiwa eneo la ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo Mnangapwani walipotembele eneo la mradi huo Agosti 19, 2019.
  • Mabalozi wakiwasili eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitope hadi Mkokotoni katika kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 31. Barabara hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu jumla ya shilingi za Bilioni 58.6