Skip to main content
News and Events

MAADHIMISHO YA TISA YA SIKU YA MARA YAHITIMISHWA WILAYANI BUTIAMA

MAADHIMISHO YA TISA YA SIKU YA MARA YAFIKIA TAMATI WILAYANI BUTIAMA

Maadhimisho ya Tisa (9) ya Siku ya Mara (Mara Day) yaliyofanyika katika uwanja wa Maria Nyerere uliopo wilayani Butiama  Mkoa wa Mara yamehitimishwa tarehe 15 Septemba, 2020. Maadhimisho haya hufanyika kila mwaka, kwa mzunguko kati ya Tanzania na Kenya kwa lengo la kuhamasisha utunzaji na Ikolojia ya Bonde la Mto Mara kwa jamii inayolizunguka bonde hilo. Madhimisho ya Mwaka huu  yameongozwa na kauli mbiu "Ikolojia ya Mara iliyotunzwa - Ustawi wetu"

Kwa kutambua umuhimu na changamoto za Ikolojia ya Bonde la Mto Mara, Baraza la Kisekta la 10 la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria, lililofanyika Kigali, Rwanda mnamo Mei 4, 2012, liliazimia na kutangaza kuwa kila tarehe 15 Septemba kuwa "Siku ya Mara", kwa kuzingatia pia katika msimu huo kuna uhamaji mkubwa wa wanyamapori kutoka Hifadhi ya Serengeti ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda Pori la Akiba la Kitaifa la Maasai-Mara katika Jamhuri ya Kenya.

Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na nchi hizi mbili Tanzania na Kenya maadhimisho ya 9 ya Mto Mara ya mwaka huu, yalipaswa kufanyika nchini Kenya, lakini kutokana na  changamoto ya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) pande zote mbili zimekubaliana kufanya maadhimisho ya siku hiyo nchini mwao. 

Madhimisho ya mwaka huu yalienda sambamba na shughuli mbalimbali kama vile, semina ya masuala ya udongo na kilimo kwa wakazi wa mkoa wa Mara waliohudhuria katika uwanja wa Maria Nyerere, Butiama, maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiliamali, maonesho ya mashamba darasa na kazi za sanaa na ubunifu. 

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima ambaye pia alikuwa  mgeni mashuhuri katika sehehe hizo amesema serikali inatambua umuhimu wa Bonde la Mto Mara katika Ustawi wa kijamii na kiuchumi kwa jamii ya pande zote mbili (Tanzania na Kenya) zinazolizunguka Bonde hilo. Sambamba na hilo Mhe. Malima amewahimiza wananchi kuendelea kutunza Ikolojia ya Bonde la Mto Mara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kushauriwa na Wataamu katika kundesha shughuli zao za kila siku kwenye mzingira yanayozunguka Bonde hilo.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Judith Ngoda akizungumza na wananchi kwenye sherehe za madadhimisho hayo amepongeza utayari    na ushiriki wa hali ya juu wa wananchi katika kulitunza Bonde la Mto Mara na kuongeza kuwa juhudi, nguvu na umoja unaoonyeshwa na Serikali za nchi zote mbili za Tanzania na Kenya unadhihirisha ushirikiano na mshikamano uliopo katika kuhakikisha ustawi wa uchumi kwa jamii inayozunguka Bonde la Mto Mara unakuwa endelevu kupitia mazingira. 

Downloads File: