Skip to main content
News and Events

MKUTANO WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 13 -15 JUNI, 2025

Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Samweli Shelukindo na Katibu Mkuu, Balozi Stephen Mbundi, wamekusanyika jijini Arusha kutathimini utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na namna ya kuboresha kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Mkutano huo unahusisha wakuu wa Idara na Vitengo utafaanuika kwa muda wa siku tatu kuanzia Juni 13, 2025.

Ikumbukwe hivi karibuni Wizara ilizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, toleo la 2024, hivyo Mkutano huo utaweka mikakati madhubuti ya kutekeleza sera hiyo kwa ufanisi zaidi ili kufikia malengo tarajiwa ya utekelezaji wa DIplomasia ya Uchumi.