DKT. MPANGO AWASILI MAREKANI KUSHIRIKI MKUTANO WA 80 Wa BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewasili jijini New York Marekani tarehe 21 Septemba, 2025 kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Dkt. Mpango anatarajiwa kuzungumza katika Mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Alipowasili jijini New York Mheshimiwa Dkt Mpango alilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dkt. Elsie Kanza, Naibu Mwakilishi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Dkt. Suleiman na maafisa Wandamizi wa Serikali.