CHINA YAISAIDIA WIZARA YA MAMBO YA NJE MILIONI 714

Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

CHINA YAISAIDIA WIZARA YA MAMBO YA NJE MILIONI 714

Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imetoa msaada wa shilingi milioni 714/- kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo msaada huo utakaotumika kuijengea uwezo Wizara ya Mambo ya Nje.

Msaada huo umekabidhiwa Wizarani na Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kukabidhi msaada huo, Mhe. Mingjian pamoja na Balozi Sokoine wamesaini Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada huo pamoja na Hati ya Makabidhiano ya msaada huo. 

Msaada huo unafuatia ahadi iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini tarehe 7 na 8 Januari 2021.

  • Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian akibadilishana Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada wa milioni 714 na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kusainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
  • Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada huo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam