Balozi Mteule wa Ufilipino awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
Balozi Mteule wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Uriel Norman Garibay akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ofisini kwake jijini Dar es Salaam.