Skip to main content
News and Events

Ziara ya Waziri Mahiga katika picha

KIKAO CHA KAZI CHA UJUMBE WA WAZIRI MAHIGA NA MHE. DKT. WILBROAD SLAA, BALOZI WA TANZANIA NCHINI NORWAY MWENYE MAKAZI YAKE NCHINI SWEDEN

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Makamu wa Rais Mtendaji wa STATOIL Bw. Lars Christian Bacher mara baada ya ujumbe wa Waziri Mahiga kuwasili kwenye makao makuu ya kampuni hiyo Oslo, Norway. Wengine kwenye picha ni Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa, Balozi wa Tanzania nchini humo, na Bw. Adamu Zuberi, mtaalam wa Wizara ya Nishati.
  • Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo. Pichani chini Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
  • Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa kwenye kikao cha kazi na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Mjini Oslo, Norway kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kwenye ziara hiyo Waziri Mahiga ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Adolf Mkenda (kulia kwa Waziri), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Bw. Jestus Nyamanga, Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati Bw. Adamu Zuberi, pamoja na maafisa waandamizi wa Mambo ya Nje.

https://foreigntanzania.blogspot.com/