Waziri Mkuu akutana na Watendaji wa Kampuni kubwa za China
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kampini ya NORINCO ya nchini China, Bw. Zhang Gaunjie alipokutana naye kwa mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini Tanzania.Mhe. Waziri Mkuu yupo nchi China kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018 jijini Beijing