Waziri Mahinga na Waziri Mambo ya Nje wa Norway
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Bi. Tone Skogen kushoto aliyemtembelea leo katika ofisi za Wizara, ambapo katika mazungumzo yao walijadili mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Norway ambapo Norway imekuwa ikisaidia katika sekta ya Nishati na Elimu hasa katika taaluma ya Uhandisi, pia ni mdau katika kupigania haki za binadamu pamoja na masuala ya jinsia.