Waziri Kabudi akutana na Balozi Al - Mashaan
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan.
Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund).
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019
Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis Ikulu Zanzibar
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)