Skip to main content
News and Events

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA WAANDAA MAONYESHO YA BIASHARA

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA WAANDAA MAONYESHO YA BIASHARA

Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umeandaa maonyesho ya biashara yanayofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 8 Oktoba, 2021 katika Kituo cha Biashara cha Wernhil (Wernhil Shopping Mall) kilichopo mjini Windhoek. Maonesho haya muhimu katika utelezaji wa Diplomasia ya Uchumi yanalenga kutangaza bidhaa za Tanzania na Utalii nchini humo ili kukuza biashara na kuvutia wawekezaji nchini. 

Katika maonesho hayo Ubalozi umewashirikisha Watanzania wajisiriamali na wafanyabiashara waishio nchini humo (diaspora) ambao wamejitokeza kuonesha bidhaa mbalimbali kama vile mchele, korosho, kahawa, asali, majani ya chai, maharagwe, vitenge, batiki, nguo za kufuma n.k.

Sambamba na kunesha bidhaa maonyesho haya yamejumuisha uuzaji wa vyakula mbalimbali vya kitanzania ambavyo vimekuwa vivutio kwa wateja wengi.

Maonesho hayo yalifunguliwa na Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba tarehe 4 Oktoba 2022.

  • 1Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi huo walipotembele maonesho ya Biashara yanayoendelea katika Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping Mall mjini Windhoek, Namibia.
  • Sehemu ya wafanyabiashara wa Kitanzania wakionesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayoendelea katika Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping Mall mjini Windhoek, Namibia
  • Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akiwasili katika Kituo cha Biashara cha Wernhil (Wernhil Shopping Mall) kilichopo mjini Windhoek, Namibia kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho ya biashara
  • Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Dkt. Modestus Kipilimba akitazama sehemu ya bidhaa za Kitanzania kwenye maonesho yanayoendelea katika Kituo cha Biashara cha Wernhil Shopping Mall mjini Windhoek, Nambia.