Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango awasili Angola
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Catumbela nchini Angola leo tarehe 04 Desemba 2024. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani, Kongo na Zambia kuhusu Ushoroba wa Lobito (Lobito Corridor), ambapo Tanzania ni mgeni mwalikwa katika Mkutano huo unaofanyika katika mji wa Lobito nchini Angola tarehe 04 Desemba 2024.