TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA BORA WAWEKEZAJI WA KIMAREKANI NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia wakati wakufunga Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani, ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani Uliopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania, ambapo alieleza kuwa Tanzania kwa sasa kuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji. Aidha, aliezea kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeweka usawa kwa kuwasikiliza wawekezaji wa Ndani na wawekezaji kutoka Nje.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akipokea nakala za vitabu vya bajeti ya serikali kutoka kwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ili kujionea mabadiliko ya uwekezaji nchini yalivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson naye akizungumza kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki (Mb.) naye akihutubia kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia kwa makini mambo yaliyokuwa yakielezwa na Prof. Palamagamb
Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Angela Kairuki pamoja na Dkt. Faraji Mnyepe wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa Mjadala wa kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye mjadala huo