Waziri Kombo Aagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameagana na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Wang Yi alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia Januari 9-10 2026. Ziara hiyo ililenga kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kihistoria na wa kimkakati kati ya Tanzania na China.
Akiwa nchini, Mheshimiwa Waziri Wang Yi alifanya mazungumzo ya uwili na mwenyeji wake Mheshimiwa Waziri Kombo na kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.










