Serikali ya awamu ya tano haichukii wawekezaji, Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yaliyopo nchini katika Sherehe za kufungua Mwaka 2019 (sherry party) zilizofanyika Ikulu, Dar Es Salaam jana. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Mabalozi wakimpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Magufuli akiendelea kuzungumza na wanadiplomasia
Kiongozi wa Mabalozi ambaye ni Balozi wa Comoro nchini, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed naye akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa.
Sehemu ya Mabalozi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (kulia)