Skip to main content
News and Events

RAIS WA UJERUMANI MHESHIMIWA FRANK-WALTER STAINMEIER AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini leo tarehe 30 Oktoba 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023, na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

  • Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) wakati alipompokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimian Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Mhe. Thomas Terstegen alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakifurahia ngoma za jadi (hawapo pichani) kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na America katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swaiba Mndeme alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasalimia Watanzania waliojitokeza kumlaki (hawapo pichani) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam