Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, amewasili nchini leo tarehe 29 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, amewasili nchini leo tarehe 29 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Rais Museveni amepokelewa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi umetanguliwa na Kikao cha Ngazi ya Juu kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye kaulimbiu isemayo "Miaka 25 ya EAC: Tafakari ya tulikotoka na matarajio ya tunapokwenda"