RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia alipowasili njini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na hadhira iliyojitokeza kwenye mapokezi ya Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na Rais huyo.
Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akizungumza na hadhira iliyojitokeza na kushiriki katika mapokezi yake wakati akiwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja
Kwa Heri, Rais Zewde karibu tena wakati mwingine nchini Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifurahia jambo wakati wa kumhaga Rais Zewde baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini.
Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akiwaaga Watanzania wakati anarejea nchini Ethiopia mara baada ya kuhitimisha ziara ya kikazi ya siku moja nchini.