Skip to main content
News and Events

RAIS SAMIA ATETA NA WANAWAKE VIONGOZI JIJINI JAKARTA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na wanawake viongozi wanaojihusisha na biashara, uwekezaji na utumishi wa umma jijini Jakarta. 

Akizungumza katika kikao na wanawake hao viongozi, Mhe. Rais Samia amewatia moyo na kuwatakaa waendelee na jitihada na harakati za kujikwamua kiuchumi ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kuleta maendeleo ya kweli kwao binafsi na nchi zao kwa ujumla.

Mhe. Rais Samia yuko nchini Indonesia kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku Tatu iliyoanza tarehe 24- 26 Januari, 2024 kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo