Rais Dkt. Magufuli apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi
Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa nchi tofauti tofauti.
Balozi wa Jamhuri ya Slovak mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Frantisek Dlhopolcek akisaini kitabu cha wageni kabla ya kukabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Slovak mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Frantisek Dlhopolcek Ikulu Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Jamhuri ya Ghana mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe.Kwame Asamoah Tenkorang akisaini kitabu cha Wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kukabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Joseph Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Joseph Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Ghana, Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana
Balozi wa Jamhuri ya Sudan mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi akisaini kitabu cha Wageni alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kukabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Joseph Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Joseph Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Sudan, Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi Ikulu Jijini Dar es Salaam