Skip to main content
News and Events

Prof. Kabudi ala kiapo cha utii Bunge la Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akila kiapo cha utii mbele ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ili kuwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo  kama Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania. Tukio hilo ambalo  limefanyika kwenye Makao Makuu  ya Bunge la Afrika Mashariki jijiji Arusha leo, limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga.

  • Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii huku Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga na wabunge wengine wakimsikiliza.Mhe. Prof. Kabudi akizungumza kwenye Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo cha utii huku Spika wa Bunge hilo, Mhe. Martin Ngoga na wabunge wengine wakimsikiliza.
  • Sehemu nyingine ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifurahia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichaniSehemu nyingine ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifurahia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi ambaye haonekani pichani