Skip to main content
News and Events

Prof. Kabudi afungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma. Ufunguzi wa ofisi hizo umefanyika tarehe 12 Aprili 2019 na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri anayeshughulikia uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki, Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Mussa Azan Zungu, Mzee Job Lusinde na Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Prof. Davis Mwamfupe. Katika hotuba yake, Mhe. Prof. Kabudi ameupongeza Ubalozi wa China hapa nchini kwa uamuzi wa kufungua ofisi hizo na kuwataka wakazi wa Dodoma na wananchi kwa ujumla kuzitumia ofisi hizo kwa ajili ya kujiimarisha kibiashara na uwekezaji.

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi kwa pamoja na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini DodomaWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi kwa pamoja na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma
  • Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo jijini Dodoma. Mhe. Wang Ke alisema kuwa ufunguzi wa Ofisi hizo ni kuunga mkono kwa dhati mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuhamia makao makuu ya nchi uliotangazwBalozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo jijini Dodoma. Mhe. Wang Ke alisema kuwa ufunguzi wa Ofisi hizo ni kuunga mkono kwa dhati mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuhamia makao makuu ya nchi uliotangazw
  • Sehemu ya viongozi waliohudhuria ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipohutubia hafla hiyoSehemu ya viongozi waliohudhuria ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipohutubia hafla hiyo
  • Sehemu ya wageni waalikwa nao wakifuatilia hotuba ya Prof. Kabudi (hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa ASehemu ya wageni waalikwa nao wakifuatilia hotuba ya Prof. Kabudi (hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi wa China jijini Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa A