Skip to main content
News and Events

Mhe. Londo Apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Tunisia

Tarehe 27 Machi, 2025 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Tunisia mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Anouar Ben Youssef.

Akipokea nakala za hati hizo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaaam Mhe. Londo ampongeza Mhe. Youssef kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuiwakilisha nchi yake hapa nchini na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itampatia ushirikiano wakati wote ili kumwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mhe. Londo amesema uhusiano bora uliojengeka kati ya Tanzania na Jamhuri ya Tunisia, unaiwezesha Sekta binafsi katika nchi hizi mbili za kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo, katika sekta ya ujenzi, kubadilishana teknolojia uzoefu na uwekezaji.

Kwa upande wake Mhe. Youssef, amesema ziara za Wakuu wa Nchi za Tanzania na na Jamhuri ya Tunisia, makundi ya Wafanyabisashara napamoja na wawekezaji zitasaidia kuimarisha uhusiano wa kidiplomaisa baina ya nchin hizo na kukuza Uchumi wa nchi hizo.