Skip to main content
News and Events

Madereva Comoro Waangazia Fursa Tanzania

Mkutano baina ya Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu na Viongozi wa Umoja wa Madereva Nchini humo ambapo viongozi hao wamefika kuangalia fursa za ushirikiano na wenzao wa Tanzania ikiwa ni pamoja na mafunzo hususan kwa vyombo mahsusi,upatikanaji wa vipuri vya magari na fursa za ajira kwa wanachama wao.

Kwa upande wake Balozi Yakubu aliwaahidi viongozi wa Umoja huo ambao unajumuisha madereva wote nchini Comoro kwa visiwa vyote kuwa watawatafutia Taasisi mahiri za udereva ili washirikiane nazo ikiwemo Taasisi za Serikali kwa mafunzo wanayohitaji.