Skip to main content
News and Events

HABARI PICHA: RAIS WA JAMHURI YA UGANDA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TATU NCHINI

HABARI PICHA: RAIS WA JAMHURI YA UGANDA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TATU NCHINI

Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda leo tarehe 29 Novemba, 2021 amehitimisha ziara yake ya kitaifa ya siku tatu nchini, na kurejea nchini Uganda ambapo ameagwa rasmi na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Geita uliopo wilayani Chato. 

Akiwa Wilayani Chato, Geita Rais Museveni amekabidhi majengo ya Shule ya Awali na Msingi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyopo katika kijiji cha Nyabilezi wilayani Chato. Ujenzi wa Shule hiyo imegharimu jumla ya Dola za Marekani Milioni 1.67, yamefanyika wakati muafaka ambapo itaongeza fursa kwa wanafunzi wote kupata elimu hata kwa wale wenye mahitaji maalum.

Rais Samia sambamba na kupokea majengo ya shule hiyo ameelezea kuwa haya ni matunda ya ushirikiano na uhusiano mzuri uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Uganda

  • Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda akimkabidhi mfano wa funguo, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya uzinduzi kama ishara ya makabidhiano ya Shule hiyo ya Awali na Msingi
  • Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika ukaguzi wa baadhi ya majengo ya Shule ya Awali na Msingi ya Museveni Pre & Primary School iliyopo Wilayani Chato, Geita
  • Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshiwa Yoweri Kaguta Museveni wakikata utepe wakati wakuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi ya "Museveni Pre & Primary School" iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita
  • Taswira ya sehemu ya jengo la Shule ya Awali na Msingi ya Museveni Pre & Primary School iliyopo Wilayani Chato, Geita
  • Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni wakiondoa kitambaa wakati wakizindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School iliyojengwa kwa msaada wa Rais Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita.