Skip to main content
News and Events

HABARI KATIKA PICHA MABALOZI WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KWA RAIS MSTAAFU MZEE MKAPA

Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wameendelea kujitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na kumuelezea kuwa ni kiongozi mahiri na msuluhishi nguli wa amani barani Afrika na duniani.
 

  • Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Dissing-Spandet akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam
  • Baadhi ya mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na mama Anna Mkapa mara baada ya kutoa salamu za pole nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
  • Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Mwakilishi wa Ubalozi wa Sudan nchini Bw. Jaafar Nasir Abdalla akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Balozi wa Zambia nchini Mhe. Benson Keith Chali akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Balozi wa Somalia nchini Mhe. Mohamed Hassan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Balozi wa Congo DRC nchini Mhe. Jean-Pierre Mutamba akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa
  • Balozi wa Hispania nchini Mhe. Fransisca Pedros akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa leo tarehe 26 Julai 2020 jijini Dar es Salaam
  • Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden nchini Bw. Michael Sulusi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa
  • Mwakilishi wa Ubalozi wa Uganda nchini Bibi. Musekura Eseza akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mzee Benjamin Mkapa