Skip to main content
News and Events

Dkt. Ndumbaro amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China Mhe. Wang Ke, katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, biashara, kilimo na teknolojia. Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro amemshukuru Mhe. Wang Ke, kwa kuendelea kuliwakilisha Taifa lake vyema hapa nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam Tarehe 25 Octoba, 2018

  • Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wang Ke (wa tatu kutoka kushoto), kulia ni maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kushoto ni Maafisa Ubalozi wa China.