Skip to main content
News and Events

DKT. TAX ATEMBELEA AICC ARUSHA AZUNGUMZA NA BODI NA WATUMISHI , NA KUZURU CHUMBA CHA ICTR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) atembelea ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo na kupanga kwa pamoja jinsi ya kutekeleza majukumu ya AICC kwa mwaka huu wa fedha na kuleta tija kwa Taifa.

Mhe Waziri katika ziara hiyo amezuru Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jingo la AICC , hospitali ya AICC, eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC) na kuzungumza na wajumbe wa bodi, menejimenti na watumishi wa AICC.

Akizungumza na watumishi hao Mhe. Dkt. Tax amewataka kuhakikisha huduma wanazotoa zinaendanana mahitaji ya wakati uliopo ili kuhimili ushindani wa soko la biashara ya utalii wa mikutano na kuiwezesha taasisi yao kupata mikutano mingi zaidi.

Mhe. Waziri pia amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuitangaza nchi pale wanapotokea kuandaa mikutano ya Kimataifa kama ilivyotokea kwa mkutano uliofanyika nchini hivi karibuni wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliojadili rasilimali watu.

Katika ziara hiyo Dkt. Tax aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bw. Ephraim Mafuru. 

Mhe. Dkt. Tax amefanya ziara ya siku moja ya kutembelea AICC kwa ajili ya kujadiliana nao na kuona ni jinsi gani wanaendana na mikakatiitakyoiwezesha AICC kuendelea kuwa Kituo bora cha Mkitano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ziara hii ni ya kwanza kwa Mhe Waziri tangu ateuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwezi Oktoba 2022. 

Kituo cha AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Taasisi nyingine ni Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam (CFR) pamoja na Mpango wa Hiari wa Kujitathmini wa Afrika (APRM).