Skip to main content
News and Events

BALOZI MUSSA AONGOZA MKUTANO WA ISHIRINI NA SITA WA KAMATI YA MAKATIBU WAKUU WA IORA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akiongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Ishirini na Sita (26) wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) unaofanyika tarehe 30 na 31 Mei, 2024 kwa njia ya mtandao ambapo ujumbe wa Tanzania umeshiriki mkutano huo kutokea Mji wa Serikali-Mtumba, Dodoma.