BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MT. LUCIA
BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MT. LUCIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ashiriki katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia iliyoandaliwa na Ubalozi wa Sweden hapa nchini. Mbali na Balozi Mulamula, Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo pia alishiriki katika hafla hiyo iliyofanyika jana jioni jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akijadili jambo na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mbunge wa Urambo (CCM), Margreth Sitta katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia