Skip to main content
News and Events

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA SAUDIA ARABIA

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akiwa nje ya jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba akizungumza na wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia aliokuja nao Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao na Mhe Waziri Mulamulajijini Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji. 

Mhe. Waziri Mulamula amekutana na Ujumbe wa wawekezaji hao ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 February 2022. Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Mhe. Ali Mwadini umeelezea utayari wao wa kuja kuwekeza nchini. 

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji nchini na kwamba Tanzania iko tayari kuwapokea.

Amesema Tanzania na Saudia zina uhusiano wa muda mrefu ambao una historia ya aina yake na kwamba uwekezaji kutoka kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

Kampuni hiyo inayomiliki viwanda mbalimbali nchini Saudi Arabia inajishughulisha na uzalishaji wa pembejeo za Killimo hususan, mbolea za kupandia na kukuzia mimea pamoja na dawa (pesticides) aina ya ‘phosphorus, nitrogen, potassium na sulfur’. 

Mbali na uzalishaji wa mbolea na dawa, Kampuni hiyo pia inazalisha vifaa vya kilimo vya plastiki ikiwa ni pamoja na khusambaza bidhaa katika nchini za Saudi Arabia, ukanda wa Mashariki ya Kati na duniani kote.

Wawekezaji hao waliwasili nchini Januari 28, 2022  wametembelea Mikoa ya Mtwara, Lindi Mtwara na Dodoma na kukutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mikoa hiyo, wadau wa sekta binafsi na wakulima wa korosho kuzungumzia biashara na uwekezaji katika nyanja hizo. 

Wawekezaji hao wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula juu ya nia yao ya kuja kuwekeza Tanzania na kutaja maeneo ambayo ni kipaumbele chao kuwa ni madini, biashara, kilimo na mifugo

  • Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (katikati) katika kikao na Wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia(hawapo pichani) kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Hemedi Mgaza na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Balozi Edwin Rutageruka wakati wa kikao na wawkezaji hao
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.Kikao hicho kilifanyika ofisini kwa Mhe. Waziri Mttumba jijini Dodoma