Wizara ya Mambo ya Nje yahamia Dodoma Rasmi
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na awamu ya pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017.
Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao.
Awamu ya pili iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi ambao waliongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katika Uhamisho huu, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara na Serikali Dodoma.
Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa ni kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole, S.L.P 2933, Jengo la LAPF, Ghorofa ya 6,
DODOMA.
Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi: +255-26-2323208,
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Tovuti: http://www.foreign.go.tz
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 27 Februari, 2017.