VIONGOZI MBALIMBALI WAENDELEA KUWASILI NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU RASILIMALI WATU
Viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika wameendelea kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu utakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam, tarehe 25 - 27 Julai 2023.
Leo tarehe 24 Julai 2023, kwa nyakati tofauti viongozi mbalimbali wamewasili nchini kushiriki Mkutano huo. Viongozi waliowasili leo ni mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel, Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone.
Wengine ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Prof. Njuguna Ndug’u, Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande pamoja na Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko.
Mbali ya Wakuu wa Nchi na Serikali, mkutano huo utawahusisha Mawaziri wa Fedha, Mawaziri wa Sekta nyingine zinazohusika na maendeleo ya Rasilimaliwatu, Watendaji Wakuu wa Benki ya Dunia na watu mashuhuri.