Skip to main content

RAIS KAGAME AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame,  awasili nchini kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili tarehe 27 - 28 April, 2023. Mheshimiwa Rais Paul Kagame na Ujumbe wake amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb.)

Katika mapokezi hayo Dkt. Tax aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

  • Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax
  • Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akipokea zawadi ya maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
  • Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akisalimiana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
  • Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku mbili