Skip to main content
Kwa Ufupi

Welcome to Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Karibu Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni wizara ya serikali inayoiwakilisha Tanzania kimataifa; kufanya diplomasia; kutengeneza Sera ya Mambo ya Nje; na kusimamia Balozi za Tanzania nje ya nchi. Wizara pia ina jukumu la kuufahamisha umma juu ya maendeleo, fursa na matarajio kuhusu mtengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na wizara nyingine za serikali. Wizara ipo katika jengo la LAPF mtaa wa Makole, Dodoma.

Kwa niaba ya serikali na watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa niaba yangu binafsi, nachukua fursa hii kuwakaribisha katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kupitia tovuti hii utaweza kupata habari mbalimbali kuhusiana na majukumu ya wizara zikiwemo taarifa kutoka katika Balozi za Tanzania Nje ya Nchi , Balozi na Nje zilizoko Tanzania, Taarifa za Biashara, Fursa za Uwekezaji, Utalii, Fursa za Ajira, Taarifa za Watanzania waishio na kufanya kazi nje ya nchi n.k.

Tovuti hii itachangia katika lengo la wizara katika kuhakikisha kwamba inakuwa daraja mahiri kati ya Tanzania na nchi zingine duniani. Tovuti hii pia itaongeza chachu ya kuimarisha na kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani.  Aidha, tovuti itatumika kama chombo muhimu katika kuimarisha hatua mbalimbali za kuwashirikisha watanzania waishio na kufanya kazi nje ya nchi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi nchini.

Karibuni Sana