Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. LEE NAK-YON awasili nchini

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) akimsuburia mgeni wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Nak-Yon akishuka kwenye ndege yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusi Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Nak - Yon yupo nchini kwa ziara ya siku tatu ambapo atafanya mkutano na mweyeji wake, kisha watasaini Mkataba wa kuondoa hitaji la Viza kwa watu wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za utumishi. Pia ataenda Ikulu kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, atatembelea Makumbusho ya Taifa, Hospitali ya Mnazi Mmoja na Kituo cha utunzaji taarifa cha NIDA kilichopo Kibaha.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. LEE NAK-YON awasili nchini

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), naye akisalimiana na Waziri Nak-Yon mara baada ya kupokelewa na Mhe. Majaliwa, wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwele naye akisubiria kusalimiana na Waziri Mkuu wa Korea.
  • Mhe. Nak - Yon akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Mhe. Matilda Masuka