Waziri Mkuu akutana na Watendaji wa Kampuni kubwa za China

Mhe. Waziri Mkuu akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kampuni ya Zinjin Gold Mine ya nchini China, Bw. George Fang ambayo imewekeza katika uchimbaji na uchakataji wa madini ya dhahabu, shaba na zinki katika nchi tisa duaniani. Kampuni hiyo imeonesha nia ya kuja kuwekeza nchini kwenye sekta ya madini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kampini ya NORINCO ya nchini China, Bw. Zhang Gaunjie alipokutana naye kwa mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini Tanzania.Mhe. Waziri Mkuu yupo nchi China kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China (FOCAC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018 jijini Beijing

  • Mhe. Waziri Mkuu akimkabidhi Bw. Gaunjie kitabu chenye taarifa kuhusu uwekezaji nchini Tanzania
  • Mhe. Waziri Mkuu akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya Syngning Guangzhou ya nchini China, Bw. WU Haineng. Kampuni ambao wana nia ya kufanyabiashara na Tanzania katika zao la mhogo
  • Mhe. Waziri Mkuu akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya GNSG ambao wana nia ya kuwekeza katika maeneo ya viwanda (Industrial Parks)
  • Mazungumzo yakiendelea