Resources » News and Events

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Vietnam na Japan waliopo nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Vietnam na Japan waliopo nchini

  • Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.